| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Gavmii mi ekuverikan matii tibegen kuriime salaam "Twasalimu taifa letu kwa umoja" | |||||
Mji mkuu | Malé | ||||
Mji mkubwa nchini | Malé | ||||
Lugha rasmi | Kidhivehi, Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri Mohamed Muizzu | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
26 Julai 1965 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
298 km² (ya 206) -- | ||||
Idadi ya watu - Julai 2018 kadirio - 2014 sensa - Msongamano wa watu |
392,473 (ya 1751) 341,356 1,102.5/km² (ya 11) | ||||
Fedha | Rufiyaa (MVR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+5) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .mv | ||||
Kodi ya simu | +960
- | ||||
1 Makadirio ya UM ya 2005. |
Maldivi ni nchi huru kwenye funguvisiwa la Maldivi katika Bahari Hindi kuanzia tarehe 26 Julai 1965.
Kabla ya hapo ilikuwa chini ya ulinzi wa Uingereza tangu mwaka 1887.
Iko km 700 kusini - magharibi kwa Sri Lanka.
Kwa jumla kuna visiwa 1,192 na kati ya hivyo takriban 200 hukaliwa na watu.
Hakuna uhakika juu ya maana ya asili ya jina lenyewe.
Wakazi karibu wote ni Waislamu; ya kwao ndiyo dini rasmi.
Lugha ya kawaida na lugha rasmi ni Kidhivehi, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Maldivi iko hatarini kupotea. Ni kwamba kimo cha juu cha nchi yake ni mita 5.1 pekee juu ya uwiano wa bahari, na wastani wake ni mita 1.5 tu. Hivyo, kama mabadiliko ya hali ya hewa kutokana kwa kupanda kwa halijoto duniani yatazidi kuleta kupanda kwa uwiano wa bahari, nchi hii yote itazama chini ya maji.