Mariah Carey | |
---|---|
![]() Mariah Carey, mnamo Mei 2013
| |
Maelezo ya awali | |
Amezaliwa | 27 Machi 1969[1] |
Aina ya muziki | R&B, pop, hip hop,[2] dance[3] |
Kazi yake | Singer, songwriter, model, record producer, actress |
Aina ya sauti | Alto[4] |
Miaka ya kazi | 1988–hadi sasa |
Studio | Columbia, Virgin, MonarC, Island |
Tovuti | www.mariahcarey.com |
Mariah Carey (alizaliwa 27 Machi 1969) ni mwanamuziki, mtunzi, mtayarishaji na mwigizaji wa Marekani.
Alitengeneza albamu yake iliyofanya vizuri katika masoko mbalimbali na chati mbalimbali mwaka 1990, chini ya studio ya Columbia Records chini ya Tommy Mottola na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kufikisha wimbo katika nafasi ya kwanza nchini Marekani. Hii ikiwa ni chati ya Billboard Hot 100. Baada ya kuolewa na Mttola mwaka 1993, mfululizo wa nyimbo bora zilimfanya moja kati ya wanamuzki bora wa Columbia na pia alikuwa anaongoza katika mauzo ya albamu mbalimbali. Kwa mujibu wa gazeti la Billboard Carey alikuwa mwanamuzi mwenye mafanikio zaidi katika miaka yab 1990 nchini Marekani [5]
Kufuatia kuachana na Mottola mwaka 1997, Carey alianza kuingiza vionjo vya hip hop katika albamu zake, na kufanikiwa kwa wastani. Umaarufu wake aulianza kuisha baada ya kuondoka Columbia mwaka 2001. Baadae alisaini mkataba na studio ya Virgin Records lakini baadae aliachishwa kutoka katika studio hizo, hii ikiwa ni baada ya kupata matatizo ya akili yaliyotangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, lakini pia ikiwa ni baada ya filamu yake ya Giltter kushindwa kufanya vizuri. Mwaka 2002 Carey alisaini mkataba na studio ya Island Records na baada ya kupata matokeo mabaya katika kipindi cha nyuma, hatimaye alirejea katika chati ya muziki wa pop,. hii ikiwa ni mwaka 2005.[6][7].
Carey ameuza nakala zaidi ya milioni 175, za albamu na single dunia nzima..[8][9][10] Carey alitajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo kwa mwaka 2000, hii ikiwa ni katika tuzo za World Music Awards.[11]. Kwa mujibu wa Recording Industry Association of America, Akiwa ameuza nakala za albamu zaidi ya milioni 62.5, Carey ndiye mwanamuziki wa kike anayeongoza kwa mauzo nchini Marekani na kushika nafasi ya 16 kwa kuuza nakala nyingi zaidi ulimwenguni.[12] . Pia anatajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo nchini Marekani katika wakati wa. Nielsen SoundScan [13]
Pia Carey aliongoza katika single za wanamuziki wanaoimba peke yao nchini Marekani.[14] kwa mwaka 2008. Carey alishika nafasi ya sita katika chati ya Billboard ya "The Billboard Hot 100 Top All-Time Artists", na kumfanya kushika nafasi ya pili kwa wanamuziki wa kike wenye mafanikio zaidi katika historia ya 'Billboard [15] Kama nyongeza katika mafanikio yake katika masoko mbalimbali, Carey pia amefanikiwa kupata tuzo za Grammy zipatazo tano. Pia anajulikana kwa sauti yake yenye uwezo wa kubadilika katika nyakati tofauti.
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)