Maryland

Sehemu ya Jimbo la Maryland








Maryland

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Annapolis
Eneo
 - Jumla 32,133 km²
 - Kavu 25,314 km² 
 - Maji 6,819 km² 
Tovuti:  http://www.maryland.gov/
Ramani ya Maryland

Maryland ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, West Virginia, Delaware, Virginia na mkoa wa shirikisho la Washington DC.

Iko kwenye pwani ya Atlantiki upande wa mashariki wa Marekani bara. Hori ya Chesapeake inagawa eneo la jimbo pande mbili.

Mji mkuu ni Annapolis na mji mkubwa ni Baltimore. Kwa miji mingine, angalia orodha ya miji.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy