Bongo kuu inayoitwa PDP-11-M7270.
Maunzingumu (pia maunzi ngumu[ 1] ; kwa Kiingereza : hardware ) ni sehemu za kompyuta zinazoshikika . Maunzingumu ni vifaa mbalimbali vinavyounda mashine ya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu:
vifaa vya kuingizia data (Input devices),
vifaa vya kutolea data (Output devices) na
vifaa katika tarakilishi (Kadi ya mtandao , Kadi ya sauti , diski kuu ).
Maunzingumu haina kazi bila programu na data za maunzilaini .
↑ Maunzingumu ni pendekezo la Kiputiputi katika kamusi ya KSK ; orodha za Microsoft na Kilinux za 2004/05 zilitumia "maunzi" pekee, ling. [https://web.archive.org/web/20120806015358/http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/documents/glossary/sw_TZ_Extended_glossary.xls
Kilinux Extended Glossary], tovuti ya Kilinux kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2009), kupitia archive.org