| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kiarabu: شرف إخاء عدل; Kifaransa: Honneur, Fraternité, Justice (Heshima, Undugu, Haki) | |||||
Wimbo wa taifa: كن للاله ناصرا وأنكر المناكر (Uwe msaidizi wa Mungu) | |||||
Mji mkuu | Nouakchott | ||||
Mji mkubwa nchini | Nouakchott | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri, serikali ya kirais Mohamed Ould Ghazouani | ||||
Uhuru - Tarehe |
Kutoka Ufaransa 28 Novemba 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,030,700 km² (ya 29) 0.03 | ||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
3,086,859 (129) 3,537,368 3.2/km² (ya 221) | ||||
Fedha | Ouguiya (MRO )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC+0) -- (UTC+0) | ||||
Intaneti TLD | .mr | ||||
Kodi ya simu | +222
- |
Mauritania ni nchi ya Afrika kaskazini-magharibi. Upande wa magharibi kuna pwani ya bahari ya Atlantiki, upande wa kusini imepakana na Senegal, upande wa mashariki na Mali na Algeria, upande wa kaskazini na Sahara ya Magharibi inayotawaliwa na Moroko.
Jina limeteuliwa kutokana na Mauritania ya kale iliyokuwa ufalme wa Waberber kusini kwa Mediteranea katika eneo la Algeria na Moroko ya leo.
Mji mkuu ni Nouakchott. Mji wa pili na kitovu cha uchumi ni bandari ya Nouadhibou karibu na mpaka wa Sahara Magharibi.