Mdudu-ute

Mdudu-ute
Mdudu-ute kutoka Ekwado
Mdudu-ute kutoka Ekwado
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila ya juu: Ecdysozoa (Wanyama wanaoambua kiunzi cha nje]]
Faila: Onychophora (Wanyama wenye matezi ya ute)
Grube, 1853
Ngeli: Udeonychophora
Poinar, 2000
Ngazi za chini

Oda 2, familia 5; spishi 29 katika Afrika:

Msambazo wa Onychophora; kijani - Peripatidae, nyekundu - Peripatopsidae
Msambazo wa Onychophora; kijani - Peripatidae, nyekundu - Peripatopsidae

Wadudu-ute (faila Onychophora, Kiing. velvet worms) ni viumbehai vinavyofanana na nyungunyungu wafupi na wanene. Wana mnasaba na vidudu-dubu na arithropodi. Jina lao linarejea uwezo wao wa kurushia ute katika vitundu viwili vya matezi nyuma ya mdomo ili kujitetea au kukamata mawindo.

Mwili wa wadudu-ute umerefuka na una pingili nyingi. Kila pingili inabeba jozi ya miguu isipokuwa pingili tatu za kichwa. Tofauti na arithropodi miguu hiyo haina viungo lakini ni kama vifuko vilivyojaa na hemolimfi (“damu”). Inaweza kusogea kwa msaada wa musuli chini ya ngozi. Kichwa kinabeba vipapasio viwili kwenye pingili la kwanza, lakini hivi havina homolojia na vile vya arithropodi. Pingili ya pili lina kipenyo kinachofanya kazi ya mdomo lakini, tena, hiki hakina homolojia na mdomo wa arithropodi. Kuna mataya (mandibili) mawili yenye ncha kali katika mdomo. Vitundu vya matezi ya ute vipo kwenye pingili la tatu.

Ngozi ya wadudu-ute ina tabaka la nje la khitini na tabaka la ndani la seli. Chini ya ngozi kuna matabaka matatu ya musuli. Nje ya ngozi inabeba nywele fupi zinazokupa hisi ya mahameli (asili ya jina la Kiingereza velvet worm).


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy