Mkimbizi

Kambi ya wakimbizi wa Rwanda nchini Zaire mnamo mwaka 1994
Wakimbizi Wapalestina wakiondoka katika vijiji vyao katika Galilaya mnamo mwaka 1948

Mkimbizi ni mtu aliyeondoka kwao kwa sababu ya kulazimishwa, kufukuzwa au kwa hofu ya kuteswa.

Kuna mapatano ya kimataifa yanayoratibu hali hiyo. Chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wakimbizi kutoka mwaka 1951, mkimbizi ni mtu ambaye (kulingana na ufafanuzi rasmi katika makala 1a ya mkataba huo), kutokana na hofu ya kweli ya kuteswa kwa sababu ya rangi, dini, utaifa, uanachama wa kikundi fulani cha kijamii, au maoni ya kisiasa, yumo nje ya nchi yake, na ameshindwa au, kutokana na hofu hiyo, hana nia ya kutegemea ulinzi wa nchi hiyo.[1]

Dhana ya mkimbizi ilipanuliwa na Itifaki ya 1967 ya Mkataba huo na mikataba ya kikanda katika Afrika na Amerika ya Kilatini kuwajumuisha watu waliokimbia vita au vurugu nyingine katika nchi zao za asili.

Wakimbizi walifafanuliwa kama kundi la kisheria katika kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakikimbia Ulaya Mashariki kufuatia Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Shirika la kimataifa linaloongoza juhudi za kuwalinda wakimbizi linaitwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (kifupi kwa lugha ya Kiingereza: UNHCR), na liliwahesabu wakimbizi 8,400,000 duniani mwanzoni mwa mwaka 2006. Hii ilikuwa idadi ya chini kabisa tangu mwaka 1980.[2]

Isipokuwa wakimbizi 4,600,000 wa Kipalestina chini ya mamlaka ya Chombo cha Umoja wa Mataifa cha Kazi ya Wokozi kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina katika eneo la Mashariki ya Karibu (UNWRA kwa lugha ya Kiingereza), ambalo ni kundi la pekee lililopewa hadhi ya ukimbizi kwa wazawa kulingana na ufafanuzi wa hapo juu.[3]

Kamati ya Marekani kwa ajili ya Wakimbizi na Wahamiaji duniani inakadiria jumla ya wakimbizi kuwa 62,000,000 na inakadiria kuwa kuna zaidi ya watu 34,000,000 waliohamishwa makwao kutokana na vita, ikiwemo wale ambao wamebaki ndani ya mipaka ya taifa.

Wakimbizi wengi ambao huhama nchi zao hutafuta ukimbizi katika nchi jirani na kwao.

"Suluhisho la kudumu" kwa idadi kubwa ya wakimbizi, kama ilivyofafanuliwa na UNHCR na serikali ni: kuwarejesha kwa hiari yao kwenye nchi zao za asili; kuwajumuisha ndani ya nchi ya ukimbizi; na kuwapa makazi katika nchi ya tatu.[4]

Kufikia tarehe 31 Desemba 2005, nchi zilizokuwa vyanzo vikubwa vya wakimbizi zilikuwa Afghanistan, Iraq, Myanmar, Sudan, na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina.

Nchi yenye idadi kubwa ya waliohamishwa makwao nchini mwao ni Sudan, ambapo idadi hiyo ni watu milioni 5 kufikia mwaka 2006, ikiwa na wakimbizi na watu wasiokuwa na makao 800,000. Wakazi wote walipohesabika, Azerbaijan ilikuwa na idadi kuu ya watu waliofukuzwa kutoka makwao ulimwenguni kote.[5]

Wakimbizi na wengineo kwa eneo miaka 2008 - 2018
Eneo
(kadiri ya Umoja wa Mataifa)
2018[6] 2017[7] 2016[8] 2014[9] 2013[10] 2012[11] 2011[12] 2010[13] 2009[14] 2008[15]
Afrika 6,775,502 6,687,326 5,531,693 4,126,800 3,377,700 3,068,300 2,924,100 2,408,700 2,300,100 2,332,900
Asia 10,111,523 9,945,930 8,608,597 7,942,100 6,317,500 5,060,100 5,104,100 5,715,800 5,620,500 5,706,400
Ulaya 2,760,771 2,602,942 2,300,833 1,500,500 1,152,800 1,522,100 1,534,400 1,587,400 1,628,100 1,613,400
Amerika ya Kilatini na KaribI 215,924 252,288 322,403 352,700 382,000 380,700 377,800 373,900 367,400 350,300
Amerika Kaskazini 427,350 391,907 370,291 416,400 424,000 425,800 429,600 430,100 444,900 453,200
Australia na Pasifiki 69,492 60,954 53,671 46,800 45,300 41,000 34,800 33,800 35,600 33,600
Jumla 20,360,562 19,941,347 17,187,488 14,385,300 11,699,300 10,498,000 10,404,800 10,549,700 10,396,600 10,489,800
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-13. Iliwekwa mnamo 2010-01-10.
  2. Refugees by Numbers 2006 edition, UNHCR
  3. "Who is a Palestine refugee?". United Nations Relief and Works Agency for Palestine Refugees in the Near East. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-02. Iliwekwa mnamo 2009-09-21.
  4. Framework for Durable Solutions for Refugees and Other Persons of Concern, UNHCR Core Group on Durable Solutions, Mei 2003, p. 5
  5. Education in Azerbaijan. UNICEF.
  6. "Global forced displacement trends. 2018 (Annexes)" (PDF). United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2018.
  7. "Global forced displacement trends. 2017 (Annexes)" (PDF). United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2017.
  8. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook" (PDF). United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2016. Iliwekwa mnamo 8 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2014. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2013. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2012. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2011. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2010. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2009. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Global forced displacement trends. (Annexes) UNHCR Statistical Yearbook". United Nations Convention Relating to the Status of Refugees. 2008. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy