Muuguzi ni mtaalamu wa afya aliyeandaliwa kupitia mfumo maalumu na thabiti wa kitaaluma, kisha kuthibitishwa na kuidhinishwa (na mamlaka iliyopo kisheria / chombo kinachosimamia taaluma hii) kutoa huduma za afya.
Muuguzi anaweza kuwa wa jinsia yoyote. Sambamba na hospitalini, muuguzi anaweza kufanya kazi maeneo tofautitofauti: nyumbani, kwenye jamii, kwenye kampuni na mashirika mbalimbali, shuleni na vyuoni.
Kazi nyingi na muhimu hutekelezwa kwa weledi mkubwa na wauguzi.