New Hampshire

Sehemu ya Jimbo la New Hampshire








New Hampshire

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Concord
Eneo
 - Jumla 24,216 km²
 - Kavu 23,227 km² 
 - Maji 989 km² 
Tovuti:  http://www.nh.gov/

New Hampshire (Hampshire Mpya) ni jimbo la Marekani upande wa mashariki-kaskazini ya nchi. Iko kwenye pwani ya Atlantiki.

Mji mkuu ni Concord na Manchester ni mji mkubwa.

Ilikuwa moja ya koloni 13 asilia za Uingereza zilizoasi dhidi ya nchi mama tangu mwaka 1776 na kuanzisha Maungano ya Madola ya Amerika.

Imepakana na Kanada, Maine, Massachusetts na Vermont.

Jimbo lina wakazi wapatao 1,315,809 (2008) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 24,217.

Kiingereza ni lugha rasmi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy