New Jersey

Jumba la Jimbo la New Jersey huko Trenton








New Jersey

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Trenton
Eneo
 - Jumla 22,588 km²
 - Kavu 19,211 km² 
 - Maji 3,377 km² 
Tovuti:  http://www.nj.gov/

New Jersey (Jersey Mpya) ni jimbo la kujitawala la Muungano wa Madola ya Amerika au Marekani. Mji mkuu ni Trenton lakini mji mkubwa ni Newark. Uko kwenye pwani ya Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara.

Impepakana na New York, Delaware na Pennsylvania. Upande wa mashariki maji ya Atlantiki.

Jimbo lina wakazi wapatao 8,682,661 (2008) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 22,608.

New Jersey ilikuwa koloni ya Uingereza tangu 1729 na pia moja kati ya koloni 13 zilizoasi dhidi ya Uingereza mwaka 1776 na kuunda nchi mpya ya Marekani tangu 1778.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy