Nyekundu

Nyekundu
( #FF0000)

Nyekundu ni moja ya rangi za pinde ya mvua. Inahesabiwa kati ya rangi kuu zinazoonekana kwa macho ya binadamu pamoja na buluu na manjano.

Nyekundu ni rangi ya jua wakati wa kuzama. Ni pia rangi ya matunda mbalimbali na rangi ya damu. Inatazamiwa kuwa pia rangi ya upendo.

Shuleni walimu hutumia mara nyingi rangi ya nyekundu wakisahihisha kazi ya wanafunzi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy