Nyoka

Nyoka
Futa
Futa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Ngazi za chini

Oda za chini 3 na familia za juu 9:

Nyoka ni watambaachi au reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani: wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.

Kama reptilia wote wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuvionda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.

Wote wanazaa kwa njia ya mayai lakini spishi kadhaa hubeba mayai ndani ya mwili hadi wadogo wamekua tayari.

Mijusi wasio na miguu wanafanana sana na nyoka lakini nyoka hawana makope machoni wala masikio ya nje.

Kuna nyoka wadogo wenye sentimita kumi tu wakiwa wazima na nyoka wakubwa hadi urefu wa mita 7.6.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy