Pennsylvania








Pennsylvania
Keystone State, Quaker State

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Harrisburg
Eneo
 - Jumla 119,283 km²
 - Kavu 116,074 km² 
 - Maji 3,208 km² 
Tovuti:  http://www.pa.gov/
Milima ya Pennsylvania.
Jumba la Uhuru lililopo Philadelphia, ambapo Azimio la Uhuru lilitungwa.
Ramani ya Pennsylvania.

Pennsylvania (pia linalojulikana kama "Keystone State") ni jimbo la kujitawala la Muungano wa Madola ya Amerika au Marekani. Ni moja ya majimbo ya kaskazini-mashariki mwa nchi, ikipakana na majimbo ya Ohio, West Virginia, Maryland, Delaware, New Jersey na jimbo la New York. Kona ya kaskazini-magharibi yagusa Ziwa Erie na Kanada iko ng'ambo ya ziwa hilo.

Sehemu kubwa ya eneo la jimbo ni milima ya Apalachi.

Mito mikubwa ni Monongahela, Allegheny na Ohio.

Mji mkuu wa jimbo hilo ni Harrisburg lakini mji mkubwa ni Philadelphia (wakazi 1,447,395 mwaka 2008). Pennsylvania pia lina miji mingine mikubwa kama Pittsburgh (316,718 mwaka 2006), Allentown (106,632), Erie (103,817 mwaka 2008), Reading (81,207) na Scranton (72,485). Kwa miji mingine, angalia Orodha ya miji ya Pennsylvania.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2020, Pennsylvania ina idadi ya watu wapatao 13,002,700 kwenye eneo la km² 119,283. Zaidi ya nusu huishi katika maeneo ya miji mikubwa Pittsburgh na Philadelphia. Kaskazini mwa jimbo watu ni wachache.

Pennsylvania ni jimbo lenye mchanganyiko wa watu wa asili mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Wazungu wa Ulaya, Waafrika wa Amerika, Wahispania, na Waasia.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy