Periheli

1. Sayari kwenye afeli yake 2. Sayari kwenye periheli yake 3. Jua

Periheli (kwa Kiing. perihelion) ni mahali katika obiti ya sayari au magimba mengine ya angani ambako ni karibu zaidi na jua. Jina linatokana na Kigiriki Περι peri (karibu) na Ήλιο "helio" (jua).

Kinyume chake ni afeli inayomaanisha sehemu ya obiti iliyo mbali kabisa na jua. Obiti ni jina la njia ya gimba kuzunguka jua.

Majina hayo hutumiwa kwa sababu obiti au njiamzingo ya Dunia si duara kamili, bali lina umbo la duaradufu. Yasingekuwa na maana kama njiamzingo ingekuwa duara kamili lakini hii haitokei hali halisi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy