Reptilia

Reptilia (Watambaachi)
Mamba ni reptilia mkubwa
Mamba ni reptilia mkubwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Watambaachi)
Laurenti, 1768
Ngazi za chini

Oda 4 (au 5) za reptilia hai:

Reptilia (kutoka Kilatini "reptilis" mwenye kutambaa; pia: mtambaazi, mtambaachi, mnyama mtambaaji[1]) ni kundi la wanyama wenye damu baridi, ngozi ya magamba badala ya nywele au manyoya wakipumua kwa mapafu. Siku hizi wataalamu hupendelea jina Sauropsida.

Wanazaa kwa njia ya mayai; wengine wanataga mayai na wadogo wanatoka nje bila ngazi ya kiluwiluwi au kwa spishi kadhaa mayai yanaiva ndani ya tumbo la mama na wadogo wanazaliwa hai.

Kibiolojia ni ngeli ya vertebrata. Jina limetokana na maumbile yao maana wanatambaa na tumbo juu ya ardhi; ama kwa miguu mifupi kama mijusi au bila miguu kama nyoka.

  1. KAST:reptile=reptilia;KKK/ESD: reptile-mtambaazi; KKK/SED: mtambaachi-reptile,snake; KKS: mtambaachi-nyoka

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy