Rivers State

Kigezo:Infobox Nigerian States

Mahali pa Rivers katika Nigeria

Rivers State ni mojawapo kati ya majimbo 36 ya Nigeria. Mji wake mkuu ni Port Harcourt.

Kusini limepakana na Bahari ya Atlantiki, Kaskazini na jimbo la Imo Abiaand Anambra, Mashariki na jimbo la Akwa Ibom na Magharibi majimbo ya Bayelsa na Delta. Kama jimbo la Delta State, Rivers State ina Waigbo wengi wa koo tofauti, lakini wengi ni wa ukoo wa Ikwerre. Pia ogoni wa Ijaw wako kwa idadi chache.

Sehemu ya ndani ya jimbo hili ina Msitu wa mvua ya kitropiki; kuelekea pwani, mazingira ya Niger Delta huwa maumbile ya mabwawa ya mangrove.

Rivers State ilikuwa sehemu ya Oil Rivers Protectorate kuanzia 1885 hadi 1893, wakati ilikuwa sehemu ya Niger Coast Pretectorate. Mwakani 1900 kanda hii ilishikanishwa na maeneo huru ya Royal Niger Company na kuunda ukoloni wa Kusini mwa Nigeria.

Jimbo hili liliundwa mwakani 1967 kwa kugawanyishwa kwa Kanda ya Mashariki wa Nigeria. Kufikia mwaka 1996 jimbo hili lilijumuisha eneo ambalo kwa sasa ni Jimbo la Bayelsa.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy