Sentimita

rula ya seremala katika mgawanyo wa sentimita

Sentimita (pia: sentimeta; kifupi: cm) ni kipimo cha urefu. Ni sawa na sehemu ya mia moja au asilimia moja ya urefu wa mita ambayo ni kipimo cha kimataifa cha SI.

Kipimo cha kulingana kwa eneo ni sentimita ya mraba (cm²).

Sentimita si kiwango rasmi katika utaratibu wa SI, lakini inafaa sana katika matumizi ya kila siku. Sentimita moja huwa ni upana wa kucha ya kidole cha mtu mzima.

millimita << sentimita << desimita << mita << kilomita


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy