Shinagimbi

Shinagimbi ni sehemu fupi ya chini ya shina la mimea fulani iliyovimba chini ya ardhi na kutumika kama ogani ya kuhifadhi chakula (wanga) ambayo mimea hiyo hutumia kuishi wakati wa baridi au hali nyingine mbaya kama ukame na joto. Mifano ni mgomba, magimbi, myugwa, uwanga na spishi za Alocasia, Sagittaria, Xanthosoma na mingi mingine.

Tofauti na kiazi ni kwamba hicho ni sehemu ya mzizi. Na tofauti na tunguu ni kwamba hilo lina majani mengi manene kama magamba.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy