Studio ya kurekodia

Mchezaji anapiga tarumpeta katika sehemu ya studio na fundi sauti anarekodi katika chumba cha dhibiti

Studio ya kurekodia ni mahali palipoandaliwa kwa kurekodi sauti hasa muziki. Studio za aina hii hutawaliwa na watu binafsi au mara nyingi na makampuni ya kurekodia yanayouza rekodi kama DVD au CD za muziki. Studio ndogo zinatumiwa pia na wanamuziki wanaotaka kuwa na kumbukumbu ya binafsi au kuuza rekodi zao wenyewe. Hapa watumiaji wanalipa kodi fulani kwa masaa ya matumizi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy