Tabasco (jimbo)

Bendera ya Tabasco
Mahali pa Tabasco katika Mexiko

Tabasco ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kusini wa nchi. Imepakana na Veracruz, Chiapas, Campeche na nchi ya Guatemala.

Tabasco inahesabiwa kuwa sehemu ya shingo ya nchi ya Tehuantepec. Upande wa kaskazini ni pwani ya hori ya Campeche

Jimbo lina wakazi wapatao 1,989,969 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 25,267.

Lugha rasmi ni Kihispania.

Mji mkuu na mji mkubwa ni Villahermosa (kwa Kihispania: kitongoji sheshe).

Gavana wa jimbo ni Andrés Rafael Granier.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy