Takwimu

Ugawaji wa watu wa Kenya kwa jinsia na umri
Ugawaji wa watu wa Denmark kwa jinsia na umri

Takwimu (kutoka Kiarabu; kwa Kiingereza: statistics) ni elimu ya data.

Data ni habari juu ya watu, nchi, uchumi, matukio au hali ya vitu mbalimbali. Takwimu inakusanya na kuangalia habari nyingi za aina hiyo ikijaribu kuzitafsiri katika namba zinazoweza kulinganishwa.

Baadaye takwimu inajaribu kutambua utaratibu ndani ya namba hizo ambazo mara zinadokeza sababu gani namba ni vile zilivyo.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy