Tanga (mji)


Jiji la Tanga
Jiji la Tanga is located in Tanzania
Jiji la Tanga
Jiji la Tanga

Mahali pa mji wa Tanga katika Tanzania

Majiranukta: 5°4′12″S 39°5′24″E / 5.07000°S 39.09000°E / -5.07000; 39.09000
Nchi Tanzania
Mkoa Tanga
Wilaya Tanga
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 393,429
Tanga mwaka 1906 hivi.

Jiji la Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi wenye Msimbo wa Posta namba 21100.

Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehemu ya kaskazini mwa Tanzania.

Njia ya reli kwenda mji wa Moshi inaanzia hapo.

Jina la mji wa Tanga linaaminiwa kutokana na lugha ya Kibondei yaani Shamba, kwa sababu wenyeji ambao walikuwa Wabondei waliishi kisiwa cha Toten lakini shughuli zao za kilimo walizifanyia eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama mji wa Tanga. [1]

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, jiji la Tanga lilikuwa na wakazi 273,332[2] walioishi katika kata 24 za eneo lake. Mwaka 2022 walihesabiwa 393,429 [3].

  1. linganisha makala "Tanga" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani
  2. "Sensa ya 2012, Tanga - Tanga CC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
  3. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy