Tanzania

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kaulimbiu ya taifa: "Uhuru na Umoja"
Wimbo wa taifa: "Mungu ibariki Afrika"
Mahali pa Tanzania katika Afrika ya Mashariki
Mahali pa Tanzania katika Afrika ya Mashariki
Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania
Mji mkuuDodoma
6°11′ S 35°44′ E
Mji mkubwa nchiniDar es Salaam
6°48′ S 39°17′ E
Lugha rasmi
Lugha za taifaKiswahili
MakabilaKupita makabila 125
Dini (asilimia)63.1 Wakristo
34.1 Waislamu
1.5 Wakanamungu
1.2 dini asilia
0.1 wengine
SerikaliJamhuri
 • Rais
 • Makumu wa Rais
 • Waziri Mkuu
 • Spika
 • Jaji Mkuu
Samia Suluhu Hassan
Philip Isdor Mpango
Kassim Majaliwa
Tulia Ackson
Ibrahim Hamis Juma
Uhuru kutoka Ufalme wa Muungano9 Desemba 1961 (Tanganyika)
10 Desemba 1963 (Zanzibar)
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 947 303[1]
 • Maji (asilimia)6.4[1]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202365,642,682[1]
 • Sensa ya 202261 741 120[2]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 84.033[3]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 1 326[3]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 227.725[3]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 3 595[3]
Maendeleo (2021)Ongezeko 0.549[4] - duni
SarafuShilingi ya Tanzania
Majira ya saaUTC+3
(Afrika Mashariki)
Muundo wa tarehesiku/mwezi/mwaka
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+255
Msimbo wa ISO 3166TZ
Jina la kikoa.tz


Tanzania (jina rasmi: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki, ndani ya ukanda wa maziwa makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi.

Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, upo kaskazini-mashariki mwa Tanzania.

Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,120[5], (nchi ya 24 duniani) kutoka 44,928,923 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2012, likiwa ongezeko la 3.2% kwa mwaka.

Msongamano ni wa watu 47.5 kwa km² (nchi ya 124 duniani).

Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 765,179), lakini Dar es Salaam ndilo jiji kubwa zaidi, lenye watu 5,383,728.

Miji mingine ni kama vile Mwanza (1,004,521), Arusha (616,631), Mbeya (541,603), Morogoro (471,409), Kahama (453,654), Tanga (393,429), Geita (361,671), Tabora (308,741) na Sumbawanga (303,986).[6]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Tanzania". The World Factbook (kwa Kiingereza) (toleo la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2024.
  2. "Idadi ya watu nchini Tanzania". Tanzania National Bureau of Statistics. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2024.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Tanzania)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Octoba 2023. Iliwekwa mnamo 14 Octoba 2023. {{cite web}}: Check date values in: |access-date= na |date= (help)
  4. "Human Development Report 2023/24" (kwa Kiingereza). Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa. 13 Machi 2024. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 22 Machi 2023.
  5. https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/
  6. Administrative Units Population Distribution Report - National Bureau of Statistics: https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy