Theluji

Maumbile ya fuweli za theluji
Nchi iliyofunikwa na theluji
Mazingira ya theluji huko Lapland, sehemu ya kaskazini ya Ufini
Mimea inayotokea wakati wa theluji kuyeyuka

Theluji (kutoka Kiarabu ثلج, thalj) ni aina ya pekee ya barafu ya maji. Inapatikana kama usimbishaji unaotelemka kwa maumbile ya barafu ya fuwelia. Fuwele za theluji ni ndogo; muundo wa fuwele unaonekana kwa macho matupu kama fuwele ni kubwa. Vipande vyake ni vyembamba sana, hivyo theluji hutelemka nyepesi si kama vipande vizito vya mvua ya mawe.

Theluji haipatikani kwa halijoto juu ya 0 . Katika Afrika inaweza kutokea tu kwenye milima mirefu kama mlima Kilimanjaro na Mlima Kenya.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy