Uhamiaji wa binadamu

Kiwango cha uhamiaji duniani.

Uhamiaji wa binadamu ni mchakato wa watu kutoka sehemu moja kwenda hadi nyingine kwa nia ya kuanzisha makazi ya kudumu au ya muda katika eneo jipya. Kwa kawaida, watu husafiri masafa marefu, ndani mwa nchi au kutoka nchi moja hadi nyingine.

Watu wanaweza kuhama kama watu binafsi, kama familia au katika makundi makubwa.[1]

Mtu anayetoroka maafa ya asilia au vita vya wenyewe kwa wenyewe huitwa mkimbizi au mkimbizi wa ndani kama anahamia ndani mwa nchi. Pia, kuna watu ambao hutafuta kimbilio kutokana na kuteswa kwa ajili ya msimamo wa siasa au dini.

Wahamahamaji hawachukuliwi kuwa wahamiaji kwa kuwa hawana nia ya kufanya makazi na kuhama kwao ni kwa msimu tu. Pia, shughuli za watu kusafiri kwa madhumuni ya utalii, upelelezi au hija si uhamiaji.

  1. "Migrations country wise". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-11. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link). One of the major migration rushes took place in the gold run in 19th century in California, Australia, and Africa.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy