Usher Raymond

Usher
Usher Raymond mnamo 2010
Usher Raymond mnamo 2010
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Usher Raymond IV
Amezaliwa 14 Oktoba 1978 (1978-10-14)
Dallas, Texas
Marekani
Asili yake Chattanooga, Tennessee, Marekani
Atlanta, Georgia
Marekani
Aina ya muziki Pop na R&B
Kazi yake Mwimbaji
Mtunzi wa nyimbo
Mtayarishaji wa rekodi
Mwigizaji
Miaka ya kazi 1994–hadi leo (anaimba)
1998–hadi leo(anaigiza)
Studio LaFace, Arista
Tovuti www.usherworld.com

Usher Raymond IV (amezaliwa tar. 14 Oktoba 1978) ni mwimbaji wa R&B-pop, mtunzi wa nyimbo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Usher. Usher, alianza kujibebea umaarufu kuanzia miaka ya 1990 hivi. Tangu hapo, ameuza albamu zake takriban milioni 35 kwa hesabu ya dunia nzima na ameshinda Tuzo tano za Grammy.[1]

Mnamo tar. 13 Septemba ya mwaka wa 2008, Usher ameorodheshwa kwenye orodha ya Wasanii Wakali 100 wa Muda Wote na gazeti la Billboard.[2] Ni miongoni mwa wasanii wachache wa lika lake kuorodheshwa katika orodha hiyo. Usher ameanzisha studio yake mwenyewe, inaitwa US Records, na pia ni mmoja kati ya wamiliki wa mradi wa Cleveland Cavaliers.

  1. "Grammy Award Winners". The Recording Academy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-11. Iliwekwa mnamo 2008-11-17.
  2. "The Billboard Hot 100 All-Time Top Artists". Billboard. Nielsen Business Media, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-25. Iliwekwa mnamo 2008-11-17.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy