Waswahili

Wanawake nchini Komoro wakiwa katika mavazi ya utamaduni wa Waswahili

Waswahili ni jina la kutaja wakazi wa miji ya pwani ya Bahari Hindi katika Afrika ya Mashariki, hasa Tanzania na Kenya, ambao ni wasemaji asili wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza.

Neno "Swahili" linatokana na Kiarabu "سواحل" (sawahil) yaani pwani, kwa hiyo maana yake ni "watu wa pwani". Lakini wanaisimu wengine wanafikiri kwamba asili ya neno hili ni "siwa hili"[1].

Siyo makabila yote ya pwani ya Afrika ya Mashariki ambao ni Waswahili, k.m. Wamijikenda.

Kimbari ni Wabantu wakichanganyikiwa kiasi na watu wengine, hasa Waarabu, zamani pia Waajemi[2].

Kiutamaduni ni Waislamu wanaofuata madhhab ya Hanafi.

Pia ni kawaida kuwaita Waswahili wasemaji wa Kiswahili hata kama ni wa makabila mengine.

"Mswahili" ni pia namna ya kumtaja mtu mjanja kwa lugha ya mzaha.[3]

  1. Mazrui, Alamin and Ibrahim Noor Shariff ,1994. The Swahili: Idiom and Identity of an African People. Trenton (New Jersey): Africa World Press
  2. Utafiti wa DNA ya watu 80 waliozikwa kwenye miji ya Waswahili kati ya mwaka 1250 hadi 1800 ulionyesha kwamba karibu nusu walitokana na Waajemi kuzaliana na Waafrika; ona: Brielle, E.S., Fleisher, J., Wynne-Jones, S. et al. Entwined African and Asian genetic roots of medieval peoples of the Swahili coast. Nature 615, 866–873 (2023). https://doi.org/10.1038/s41586-023-05754-w
  3. "Waswahili ni Akina Nani?". Google Arts & Culture. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy