Kinyakyusa

Kinyakyusa (au Kinyekyosa; pia huitwa Kingonde) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanyakyusa wanaokaa hasa Rungwe. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kinyakyusa imehesabiwa kuwa watu 805,000. Pia kuna wasemaji 300,000 nchini Malawi.

Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyakyusa iko katika kundi la M30.Na asili ya jina hilo la wanyakyusa ni kutokana na jina la mke wa mtawala wa kimila au chifu aliyeitwa kyusa, pia awali waliitwa wasokile hiyo ni kutokana na salamu yao asali aliyosema sooki sooki nna!


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy